Tuesday, August 27, 2013

Rennender Gepard (Foto: Fotalia)DUMA.
Hakuna anayekimbia kwa kasi zaidi yake: duma wanaweza kufikia kasi ya hadi kilomita 120 kwa saa. Ni jambo linaloendana na mazowea yao ya kuwinda. Wanyama hao huwinda mchana, ambapo wanamnyemelea mnyama mwingine na kisha kukimbia kwa kasi na kumkamata kwa kushtukiza. Hata hivyo hawawezi kukimbia kwa muda mrefu na hivyo wasipomkamata swala baada ya mita kama mia moja wanakata tamaa.Gabelbock (Foto: Getty Images)SWALA"Pronghorn" Hakuna anayekimbia kwa muda mrefu kama yeye: Pronghorn wanafikisha kasi kati ya kilomita 60 hadi 70 kwa saa na wanaweza kukimbia umbali wa kilom
ita tano. Mwili wao umezoea kukimbia mwendo mrefu kwa sababu moyo wao kwa mfano una ukubwa mara mbili ya ule wa kondoo. Faida yake ni kwamba wanaweza kuwakimbia wanyama wengine wanaotaka kuwakamata.Zwei Straußenvögel. (Foto: AP Photo/Jerome Delay) MBUNI
Hakuna ndege anayekimbia kwa kasi zaidi yake: Kwake si tatizo kukimbia kwa kasi ya kilomita 70 kwa saa. Anaweza kukimbia kwa nusu saa kwa kasi ya kilomita 50 kwa saa. Ana miguu mirefu na misuli inayofaa kwa kukimbia. Mbuni ni ndege pekee mwenye vidole viwili tu miguuni. Lakini licha ya kuwa na mabawa makubwa, mbuni hawezi kupaa kwa sababu ya uzito wake. Sperbergeier Weltvogelpark WalsrodeTAI.
Hakuna anayepaa juu zaidi yake: Mwaka 1973 ndege wa aina hiyo aligongana na ndege ya kubeba abiria iliyokuwa ikiruka mita 11,200 juu ya usawa wa bahari. Aina nyingine za ndege zinaweza kupaa kufikia mita 100 hadi 2,000 tu. Lakini wapo pia ndege wanaolazimika kusafiri umbali mrefu hali ya hewa ikibadilika na hao wakati mwingine hupaa mita 9,000 angani. Kwa mfano wakivuka milima ya Himalaya. Puma, Belgrade ZooPUMA.
Hakuna anayeruka juu zaidi: Licha ya kuwa na uzito wa zaidi ya kilo 50, puma wanaweza kuruka juu urefu wa mita tano na nusu na kurukia mti. Urefu huo unaweka rekodi kwa wanyama wanaonyonya na waishio ardhini. Pomboo ni samaki pekee anayeruka juu zaidi kwani yeye anafikia mita saba.Kolibri in KalifornienNDEGE mdogo "Hummingbird"
Hakuna aliye mdogo zaidi: Jamii nyingi za ndege wa hummingbird ni wadogo sana na ndio wanaoshikilia rekodi ya kuwa ndege wadogo zaidi duniani. Wana urefu wa sentimita sita tu na uzito wa gramu mbili. Wakiwa wanapaa, mabawa yao yanapiga mara 40 hadi 50 kwa sekunde.Flash-Galerie Film Unsere OzeaneNYANGUMI.
Hakuna anayezama chini zaidi: Nyangumi huyu ni mnyama pekee anayenyonya mwenye kuweza kuzama chini na kufikia kina cha mita 3000 na kubakia majini kwa saa nzima. Hili linastaajabisha sana kwani nyangumi lazima wavute pumzi. Mbinu yao ni kupelea damu katika viungo muhimu tu wakiwa majini, yaani katika moyo na kwenye ubongo.Oryx AntilopenCHOROA.
Hakuna anayestahili joto zaidi yake: Joto la mwili la nyuzi joto 45 halimsumbui. Binaadamu angekuwa ameshakufa kwenye joto kama hilo. Siri yao ni kuwa na mishipa mingi ya damu katika shingo inayopooza mwili. Pamoja na hayo, choroa hawahitaji kunywa maji mengi, mara moja kwa wiki kadhaa inatosha.Bildergalerie bedrohte Tier- und Pflanzenarten Fledermaus POPO.
Hakuna anayesikia vizuri zaidi: Popo wana masikio yanayosikia vizuri kuliko wanyama wengine wote. Wakiwa wanapaa usiku, hutoa milio isiyosikika kwa sikio la binadamu. Masikio yao hugeukia mwangwi wa sauti hiyo na kwa njia hiyo wanaweza kuwakamata wadudu hata panapokuwa na giza totoro.Rätsel um Sprungkunst der Flöhe gelöstCHAWA. Bingwa wa kuruka juu. Chawa anaweza kuruka urefu ulio hadi mara 200 ya ukubwa wake mwenyewe. Ipo aina moja ya chawa inayofikisha hadi mara 400 ya ukubwa wake.

0 comments:

Post a Comment