VIDEO Queen wa wimbo wa Masogange wa Belle 9, Agnes Gerald
‘Masogange’ amejikuta mikononi mwa Waziri wa Uchukuzi, Dr. Harrison
George Mwakyembe akichukua dakika kadhaa kumzungumzia huku akiwa
ameshika iPad yenye picha za msanii huyo.
Akizungumza na mapaparazi ofisini kwake jijini Dar, Agosti 16, 2013 wakati akitaja majina ya maafisa wa mtandao wa wauza madawa ya kulevya ambayo ni wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Mwakyembe alisema anawashangaa waliomruhusu msanii huyo kupita na mzigo wa unga.
Huku akionesha hamjui vizuri Masogange na kusema aliimbwa kwenye wimbo mmoja, Mwakyembe alisema siku ya tukio msanii huyo na mdogo wake walinaswa na CCTV za uwanjani hapo wakiwa na mfanyabiashara mmoja ambaye ameagizwa akamatwe.
Alisema kamera hiyo ya CCTV iliweza kuwaona akina Masogange hadi wanaingia kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.
Muda mwingine Mwakyembe aliionesha picha ya Masogange akiwa ameshika noti za nchi tatu, Afrika Kusini, Tanzania na dola za Marekani.
Kumbukumbu za haraka zinaonesha kuwa, ishu ya Masogange kunaswa na madawa ya kulevya Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu imekuwa ‘hoti’ zaidi kuliko Watanzania wengine.
Waziri Mwakyembe aliagiza maofisa wanne ambao walikuwa zamu siku ya Julai 5 katika Uwanja wa JNIA ambao ni Yusuph Issa, Jackson Manyoni, Juliana Thadei na Mohamedi Kalungwana kufukuzwa kazi mara moja kwa vile wao ndiyo walikuwa zamu wakati Masogange na mwenzake, Mellisa Edward wakipita na ‘mzigo’ huo.

salut;global publisherz
0 comments:
Post a Comment