Wednesday, August 28, 2013

 KWA muda mrefu, zilisikika sauti za kupiga vita makundi ya wanawake yaliyosifika kwa kucheza utupu kwa kulowanisha khanga maji maarufu kama Khanga Moko Ndembendembe lakini sasa imeibuka nyingine, inayoitwa Fulana au Tisheti Ndembendembe
Uchunguzi wetu wa miezi kadhaa tangu mwaka jana ulibaini kwamba tayari staili hiyo ya uchezaji wa muziki wa mwambao kwa kulowanisha tisheti laini nyeupe kwa maji na kusababisha chuchu kuonekana sawia, inazidi kushika kasi kama moto wa kifuu Bongo.
Ilibainika kuwa staili hiyo ambayo ilianzia Pwani ya Kenya, sasa inatumiwa kudhalilisha warembo Uswahilini hasa kwenye ngoma maarufu za ‘kigodoro’ ambazo huchezwa bila kujali rika mbalimbali zinazokuwa zimechanganyikana. Habari zilisema kuwa katika uchezaji huo, sharti ‘nido’ ya mrembo iwe saa sita ili kuwavutia na kuwaridhisha wanaume kimahaba ambao kazi yao huwa ni kuwatuza fedha baada ya kufurahishwa kwa kutazama uchezaji huo na wengine kuondoka nao kwenda kuvunja amri ya sita.
Ilifahamika kuwa staili hiyo imewavutia wengi na vikundi vya uchezaji huo vimeanza kuundwa japo havijapata umaarufu mkubwa.
Mamlaka na wizara husika zinatakiwa kukemea kwa nguvu zote kwani huo ni mwanzo mwingine wa mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania na ongezeko la maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

0 comments:

Post a Comment