Friday, September 6, 2013

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, ameshare picha zinazowaonesha akiwa na mwanae pamoja na mama wa mtoto wake huyo, Faiza Ally, waliamua kupark usafiri wao pembeni ya barabara na kufurahia mandhari ya kuvutia ya Mlima Kitonga, mkoani Iringa. Tazama picha zao.
946294_484823404924724_125451513_n
Faiza na mwanae
Faiza na mwanae
935165_484821214924943_1643712272_n
Sugu na familia yake
Sugu na familia yake
chanzo:jambo tz

Saturday, August 31, 2013

Gari lililokuwa limembeba Lulu likiingia Ukumbini hapo.
Lulu akishuka ndani ya gari hilo tayari kwa kuzama ukumbini. Lulu akiingia ukumbini
Msanii wa Orijino Komedi Lucas Mhuvile 'Joti' (katikati), akishuhudia uzinduzi huo na marafiki zake.
Lulu akiongea jambo muda mfupi kabla ya uzinduzi wa filamu hiyo.
Wema  na Kajala wakiselebuka moja ya ngoma za Lady Jaydee mala baada ya kuanza kutumbuiza.
Lulu akiimba wimbo wa Yahaya sambamba na Lady Jaydee.
Baadhi ya mashabiki walihudhuria kwenye uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini.
Barnaba akinogesha uzinduzi huo kwa kuchalaza gitaa.
MSANII wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo amefanikisha zoezi la uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Foolish Age Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa tasnia mbalimbali hapa Bongo, wakiwemo; Judith Wambura 'Lady Jaydee', ambaye alitumbuiza sambamba na Barnaba na Amini.
(HABARI/PICHA: MUSA MATEJA NA SHAKOOR JONGO/GPL)
Huu ujumbe wa “Birthday” wa Nisha kwa Hemedy wazua maswali yasiyo na majibu

Leo mwigizaji Hemedi Suleiman maarufu kama Hemedy PHD anasherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 27 katika ulimwengu huu.

Huku akimiminiwa salamu nyingi sana za pongezi na fans na wadau mbalimbali nchini. Moja ya salamu zilizomfikia mkali ni kutoka kwa mwanadada Nisha Jabu, ambaye aliamua kufunguka yafuatayo na kuacha watu wakiwa na maswali bila majibu kuhusu alichokiandika.



HAPPY BIRTHDAY.. mwanaume unaefanana na mwanaume wa maisha yangu, mwanaume nnaempenda kuliko chochote duniani,mwanaume alienifanya nisione mwingine duniani zaidi yake,mwanaume akiyenipunguza kilo kumi ndani ya siku 20,(mind ur own bizzness usiniulize kwanini), ninapokuangalia ww namuona yeye,, HAPPY BIRTHDAY my Lusungu my Fernandoo .. my Mathias,, maisha mema na yenye baraka tele yawe mbele na nyuma yako..



Huo ni ujumbe alioundika mwanadada huyu kwa Hemedy.

Happy birthday Hemedy
Tabia mbaya! Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.
 Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.
Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani.
 Shushushu wetu aliwapiga chabo ‘wakifanya yao’ hadi Diamond alipokwenda stejini na kuangusha bonge la shoo huku akimwacha Linah mpweke.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.

Taifa la China halina mzaha mbele ya biashara haramu ya madawa ya kulevya na kwa kutambua kwamba wanaohusika zaidi ni Waafrika, sasa hivi kila mja mwenye ngozi nyeusi aliyepo nchini humo, anapewa msoto wa nguvu.

Wabongo wanaoishi China, kwa sasa wanahenyeshwa isivyo kawaida katika msako uliopewa jina
na Watanzania kwamba ni Oparesheni Safisha Wauza Unga.
Katika hoteli wanazofikia, vijiwe vyao, barabarani na kadhalika, kote huko wanapewa msoto wa guvu kwa kile kinachoelezwa kuwa Wachina hawana imani tena na Watanzania na Waafrika kwa jumla ama wanaoishi nchini humo au hata wale wanaoingia na kutoka.

“Wazungu wa unga (wafanyabiashara wa madawa ya kulevya) wanatuharibia starehe hapa China, hatuishi kwa amani tena. Mtu unaweza kukaguliwa siku nzima kisa eti wanawatafuta wanaouza unga,” alisema Artides Kimota ambaye ni Mtanzania anayeishi China kwa sasa.
Aliongeza: “Unajua sasa hivi China imekuwa na uingizwaji mkubwa wa madawa ya kulevya. Kwa Serikali ya China hii ni kashfa nzito. Kwa vile wanajua Waafrika ndiyo sababu kuu, sasa hivi kila Mwafrika anapewa msukosuko.
  “Kwa kweli ukiwa Mwafrika hapa China ni mateso makubwa sana kwa sasa. Kuna agizo la serikali ambalo limelitaka jeshi la polisi hapa China kuhakikisha madawa ya kulevya yanatokomezwa na wahusika wanakamatwa.

“Kila anayekamatwa na madawa ya kulevya au na kitu chochote ambacho siyo halali, anafunguliwa mashtaka.


 Mimi naishi kwenye Jiji la Qingyuan, nimeshahuhudia Mtanzania mmoja, Wanigeria wawili na Waghana watatu wakikamatwa.

“Kote hakuna kupumua, hata huko Guangzhou, Beijing na kwingineko kunatisha kwa msako. Nasikia kwenye Mji wa Shanwei alikamatwa Mtanzania mwingine, akakutwa na ungaunga wa marumaru ambao alikuwa nao kama sampuli kwa ajili ya biashara zake, alikamatwa lakini aliachiwa baada ya kupimwa na kugundulika siyo madawa ya kulevya.”

Habari zaidi zinasema kuwa pamoja na sifa mbaya ya Watanzania nchini humo lakini imebainishwa kwamba Wanigeria ndiyo kundi hatari na wanawindwa zaidi kwa sababu raia wa nchi hiyo wameshachafuka sana.  


Imebainishwa zaidi kuwa kwa vile siyo rahisi kumtofautisha Mnigeria na Waafrika wengine kwa haraka, ndiyo maana kila Mwafrika anapoonekana ni lazima ale msoto wa kukaguliwa ili kuhakikisha kama ana ‘mzigo’ au hana.


Risasi Jumamosi linamiliki picha zinazowaonesha baadhi ya Waafrika wakiwa chini ya ulinzi, wakitembezwa vifua wazi, kueleka vituo vya polisi kufunguliwa mashtaka ya uhalifu mbalimbali ikiwemo madawa ya kulevya.

KINACHOWAPONZA NI HIKI
Kwa mujibu wa taarifa kutoka China, taifa hilo limeshtukia kwamba pamoja na sheria kali za udhibiti wa madawa ya kulevya zilizopo na adhabu kali ikiwemo ile ya juu kabisa ya kunyongwa hadi kufa kwa mtu anayekutwa na hatia ya kujihusisha na biashara hiyo, polisi wameendelea kupigwa bao la kisigino.


Imeelezwa kwamba watu wanaosafiri na madawa ya kulevya tumboni, maarufu kama punda ndiyo wanaofanya madawa yazagae nchini humo.


“Punda ndiyo wanatuponza, Serikali ya China imeshtukia kuona kwamba madawa yapo sana mitaani, kwa hiyo kukomesha kabisa hilo, wanafanya msako hatari sana. 


Wakifika chumbani kwako utajuta, wanapekua kila upande wa chumba.

“Vilevile ikitokea mtu anawasili uwanja wa ndege akiwa dhaifu, anafuatiliwa sana. Asikwambie mtu, hakuna Mwafrika aliyepo China anayeishi kwa raha, iwe unauza au huuzi lazima uhenyeshwe,” alisema Dominick Rafiki anayeishi Guangzhou, China.

CHINA YASISITIZA KUENDELEA KUNYONGA
Ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International mwaka 2012, iliitaja China kama taifa kinara kwa kunyonga watu wenye makosa mbalimbali na kuitaja nchi hiyo kama katili zaidi duniani.


Amnesty International inapingana na adhabu ya kifo, kwa hiyo imekuwa ikitumia jitihada mbalimbali kuhakikisha linaishawishi China iachane na hukumu za kunyonga watu bila mafanikio.

Shirika hilo lilieleza kwamba China imeendelea kuweka msisitizo wa kunyonga watu, huku ikiwa na rekodi ya kunyonga maelfu ya watu kila mwaka.
BALOZI AKIRI HALI NI MBAYA
Balozi mpya wa Tanzania nchini China, Luteni Jenerali Mstaafu, Abdulrahman Shimbo amekiri kwamba hali ni mbaya kutokana na wimbi kubwa la Watanzania kukumbwa na kashfa ya madawa ya kulevya, huku wengine wakiwa wameshahukumiwa kunyongwa.


“Ni kweli hali ni mbaya, kuna vijana wetu wengi wanaipa sifa mbaya nchi yetu hapa. Kama inavyofahamika, mimi bado mgeni lakini nikipewa muda kidogo nitakuwa na ripoti kamili ya jinsi Watanzania wanavyohusishwa na hii biashara haramu ya madawa ya kulevya,” alisema Balozi Shimbo ambaye alikuwa Mnadhimu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)
source;http://paparaziblog.blogspot.com/2013/08/picha-wabongo-china-wahenyeshwa.html?spref=fb

Friday, August 30, 2013


Na Imelda Mtema
Baada ya hivi karibuni kuandikwa habari iliyoeleza kwamba nchini Kenya kuna demu aliyemzimikia ile mbaya mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku akiahidi kumpa penzi zito, mpenzi wa msanii huyo Peniel Mwingilwa ‘Penny’ ameibuka na kudai hatishwi na maneno hayo.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Penny ambaye sasa anapika na kupakuwa kwa Diamond alisema anamuamini sana mpenzi wake huyo na kwamba kuhusishwa kwake na mambo ya mademu kila kukicha kunatokana na kazi yake.
“Yatasemwa mengi lakini siwezi kumuacha Diamond, namuamini na najua haya yote yanayotokea ni kwa sababu ya kazi yake kwa hiyo wanaodhani mimi nitayachukua na kuamua kumuacha watasubiri sana, ndiyo kwanza penzi letu linazidi kushamiri,” alisema Penny.
chanzo;GPL
Diamond na vijana wake wakitoa burudani kwa mashabiki.
...Akiangalia mashabiki wake.
 
Mkurugenzi wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka (mwenye gauni jekundu) akiwa  na mama mzazi wa Diamond.
Meneja wa Diamond, Babu Talle, mwenye fulana aina ya Form Six na kiongozi wa kundi la Wanaume Family, Said Fella, anayeonekana akisoma sms kwenye simu, wakifuatilia maelezo hayo ya Diamond.
Madam Ritha na Nay wa Mitego  walikutana uso kwa uso ikabidi wapige picha ya pamoja.
Meneja wa kampuni ya Global Publishers, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’ (mwenye tai katikati) akiwa na wasanii wa Bongo Fleva, Dully Sykes na Ommy Dimpoz.
 
UZINDUZI WA video mpya ya Nasib Abdul ‘Diamond’ iitwayo My Number One, imeonekana kufuru kutokana na maandalizi yake na aina za kamera zilizotumika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi rasmi wa video hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar, walisema kuwa Diamond ameleta mabadiliko katika tasnia hiyo ya muziki wa Bongo Fleva hasa katika kipengele cha video bora.  Maandalizi ya video hiyo yamegharimu kiasi cha Dola za Kimarekani 30,000 ambazo ni kama sh. Milioni 48.5.