Thursday, August 29, 2013


Na Musa Mateja
WANAMUZIKI wapendanao waliomwagana miaka kadhaa iliyopita, Estalina Sanga ‘Linah’ na Amini Mwinyimkuu wamejikuta wakidendeka hadharani baada ya utamu wa muziki kuwakolea.
Estalina Sanga ‘Linah’ na Amini Mwinyimku wakidendeka hadharani.
Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita wakati mastaa hao walipokuwa wakipafomu katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ‘Noma Sana’, katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora.
Walipokuwa wakiimba pamoja wimbo wa Mtima Wangwe, ndipo wawili hao walipong’ang’aniana staili ya kumbikumbi na kuanza kudendeka huku watu wakishangilia.
Linah na Amini wakiwa kimahaba.
“Jamani hawa bado wanapendana, si bora warudishe penzi lao. Mbona wamependezana,” alisikika mdau ingawa wenyewe hawakutaka kulizungumzia suala hilo.

0 comments:

Post a Comment