Stori: Waandishi Wetu
AMA
kweli hiki ni kioja kwa mwaka 2013 ambapo wanawake wanaofanya biashara
haramu ya kuuza miili (makahaba) jijini Dar wameunda umoja wao na kutoa
bei elekezi ya kutisha katika huduma yao.
Uchunguzi wa waandishi wetu
kupitia Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers
umebaini kuwa umoja huo unaitwa UMADA (Umoja wa Makahaba Dar).
Katika
makubaliano yao, kuna mambo ya kushangaza ikiwa ni pamoja na kujipangia
bei ya pamoja na kupanda kwa kasi ya ajabu kwa bei ya huduma
inayotolewa na wanawake hao sehemu mbalimbali jijini Dar huku
watakaojiuza bei chee wakiambiwa watakiona.
Maeneo ambayo yalifikiwa na OFM na kupewa utaratibu wa huduma ni kama ifuatavyo;
Maeneo ya Jolly Club, Upanga, Dar ilibainika kuwa fastafasta ni Sh. 30,000 na kulala usiku kucha ni Sh. 100,000.
Maeneo
ya Afrika Sana, Sinza, Club Sun Cirro, Ubungo na Club Meridian,
Kinondoni, huduma ya fastafasta ni Sh. 10,000 na kulala ni 40,000.
Maeneo
ya New Maisha Club, Masaki ni kati ya dola 50 (Sh. 80,000) kwa
fastafasta na dola 100 (Sh. 160,000) kulala kwa Mzungu na kwa Mswahili
ni Sh. 50,000 kwa huduma ya haraka na Sh. 100,000 kulala.
Maeneo ya
Meeda Club, Sinza kuna huduma ya fastafasta tu ambayo hutolewa kati ya
Sh. 5,000 had 10,000 huku huduma ya kulala ikifutwa kwenye bajeti ya
mwaka huu kwani eneo hilo wapo wengi hadi wanaovaa kandambili.
Huko Uwanja wa Fisi huduma hupatikana kuanzia Sh. 500 hadi 5,000 huku maeneo ya Buguruni ikianzia Sh. 2,000 hadi 10,000.
Katika
massage centers (maduka ya kuchua mwili), ilibainika kuwa bei ni kati
ya Sh. 50,000 hadi 100,000 kutegemea na kiwango cha mrembo.
Ilifichuka
kuwa kwa wale wa maofisini wanaojishughulisha na biashara hiyo kwenye
vituop vya ‘masaji’, bei ni kuanzia Sh. 100,000 kwa siku nzima na ni
warembo wa haja.
Huko Temeke, Dar ilibainika kuwa wapo hadi wa Sh.
200 huku wale wa vyuo mbalimbali wakianzia Sh. 5,000 hadi 15,000 ambao
wengi hupatikana klabu za starehe usiku hasa ‘boom’ likikatika.
Kwa wale wa vyuoni ilibumburuka kuwa mwanaume akiwa na gari ana uwezo wa kumchukua yule anayemtaka bila kipingamizi.
Katika
mahojiano na timu yetu, baadhi ya wanawake hao walifunguka kuwa
wamefikia hatua hiyo ya kupandisha bei maradufu kwa sababu kila kitu
kimepanda bei kuanzia mavazi, sabuni, vipodozi na nauli hivyo nao ili
kuboresha huduma lazima bei ipande.
Gazeti hili linakemea vikali bishara hiyo haramu na kuviomba vyombo husika kuingilia kati ili kuikomesha.
Monday, August 26, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment