
Na Imelda Mtema Baada ya hivi karibuni kuandikwa
habari iliyoeleza kwamba nchini Kenya kuna demu aliyemzimikia ile mbaya
mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku akiahidi kumpa penzi zito,
mpenzi wa msanii huyo Peniel Mwingilwa ‘Penny’ ameibuka na kudai
hatishwi na maneno hayo.

Akizungumza
na Ijumaa hivi karibuni, Penny ambaye sasa anapika na kupakuwa kwa
Diamond alisema anamuamini sana mpenzi wake huyo na kwamba kuhusishwa
kwake na mambo ya mademu kila kukicha kunatokana na kazi yake.

“Yatasemwa
mengi lakini siwezi kumuacha Diamond, namuamini na najua haya yote
yanayotokea ni kwa sababu ya kazi yake kwa hiyo wanaodhani mimi
nitayachukua na kuamua kumuacha watasubiri sana, ndiyo kwanza penzi letu
linazidi kushamiri,” alisema Penny.
chanzo;GPL
0 comments:
Post a Comment